Kusafiri na watoto katika magari

Sheria ya Australia inahitaji watoto wote wenye umri chini ya miaka 7, lazima kutumia kiti cha watoto wakati wa kusafiri katika gari. Hii ni kulinda mtoto kutojeruhiwa wakati kunakotokea ajali ya gari.

Aina ya kiti cha mtoto kinatakiwa kinatokana na miaka na ukubwa wa mtoto. Kiti cha mtoto kinatakiwa kurekebishiwa ili kuenea mtoto kwenye gari, na kufungwa vizuri, na kimeenea katika gari.

Watoto wa miezi 0-6

Lazima kusafiri kwenye kiti ambacho kimefungwa kinachoangalia nyuma. Kiti hicho kinatakiwa kuwa kwenye viti vya nyuma – SI viti vya mbele.

Watoto wa miezi 6 – na miaka 4

 • Wanaweza kusafiri kwenye kiti ambacho kinaangalia nyuma au mbele, chenye mikamba, na kutokana na ukubwa wao. Mtoto anapaswa kusafiri kwenye kiti cha nyuma - SI kiti cha mbele.
 • Sasa kuna viti vya watoto ambavyo vina mikanda, kwa watoto wa miaka 8.

Watoto wa miaka 4 hadi angalau miaka 7

 • Wanaweza kusafiri kwenye kiti ambao kinaangalia mbele au kiti cha nyongeza, inatokana na ukubwa wao. Kiti cha nyongeza (booster seat) kinainua mtoto hadi nafasi nzuri ili mikanda ya gari kumuenea.
 • Watoto wa umri wa miaka 4-7 wanaweza kusafiri kwenye kiti cha mbele (kwa kutumia kiti cha nyongeza) kama viti vyote vya nyuma vinatumiwa na watoto wa myaka chini ya 7.
 • Viti vya nyongeza vyenye Kamba ya nyuma na juu vina ulinzi nzuri kuliko aina nyingine vya viti hivyo.
 • Watoto wanastahili kutumia kiti cha nyongeza mpaka wanafika urefu wa 145 cm. Kama wanatumia mikanda ya viti vya watu wakubwa, watakuwa katika hatari kubwa ya kujeruhiwa kama ajali inapotokea.

Kufaa kwa kiti cha nyongeza

Kila siku fuata maelekezo ya mtengenezaji unapoweka kiti cha mtoto au kiti cha nyongeza katika gari lako.

Kwa watoto wa miaka chini ya 4 < 1, kufaa kwa kiti kinamaanisha:

 • Kiti kinawekwa katika gari kwa kupitisha mikanda kwenye pahali pa alama na kuifunga.

Kwa watoto Zaidi ya miaka 4, wanasafiri kwa kiti cha nyongeza:

 • Kama kuna mkanda wa juu, funga kwenye gari.
 • Mkanda unatakiwa kuzunguka mtoto na kufungwa.
 • Mkanda wa juu unafungwa kwenye gari.

Kuchagua kiti

Kiti cha mtoto na kiti cha nyongeza vinavyoruhusiwa kutumika ni vile vilivyo na viwango vya usalama wa Australia (AS / NZS 1754). Hii ina maana kuwa viti vya gari vinavyonunuliwa nje ya Australia hairuhusiwi.

Jaribu kutotumia viti ambovyo vilishatumika vinaweza kuwa vimeharibika na havitakua salama.

 • Mikanda inafungwa ili kumshika mtoto kwenye kiti.

Kuna faini kubwa na pointi zinazotolewa kutoka leseni kwa kutotumia viti vya watoto. Faini hizi zinatumika kwa kila mtu katika gari ambaye hakutumia kiti sahihi.